Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TFF YASHUKURU WALIOKUJA MPOKEA SAMATA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza us...

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na
wadau wa mpira wa miguu Tanzania
waliojitokeza usiku saa 8 uwanja wa ndege wa
JK Nyerere kumpokea mchezaji bora wa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza ndani Mbwana
Samatta.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK
Nyerere, Samatta alipokelewa na viongozi wa
serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na
mama yake mzazi na watanzania wengi
walijitokeza kumlaki mchezaji huyo.
Mara baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege,
TFF ilimpeleka moja kwa moja kupumzika
katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta
jijini Dar es salaam, ambapo imemlipia
gharama ya kukaa kwa siku mbili.
Akiwa hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Michezo, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana
Yassoda alitoa salamu za pongezi kwa niaba
ya Serikali, kisha mchezaji alipata nafasi ya
kuongea na waandishi wa habari.
Kwa kuwa Jumanne, Januari 12 ni Sikukuu ya
Mapinduzi, na Janauri 13 ni fainali ya kombe
la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, siku ya
Alhamisi Januari 14 TFF imeandaa dua
maalumu ya kumpongeza Samatta
itakayongozwa na viongozi wa dini mbalimbali
katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11
jioni.
Hata hivyo ratiba zingine za kumpongeza
Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa na
wadau wengine zinaweza kuendelea ilimradi
TFF ijulishwe mapema kwa ajili ya kuratibu
uwepo wa mchezaji mwenyewe.
IMETOLEWA NA TFF

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top