MABINGWA wa Germany Bayern Munich Leo wakiwa kwao Allianz
Arena Jijini Munich wameitandika Borussia Dortmund Bao 5-1 kwenye Mechi
ya Bundesliga ambayo Jina lake la Ubatizo ni Der Klassiker.
Hadi Mapumziko Bayern walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Thomas Muller, moja likiwa la Penati.
Kipindi cha Pili Straika hatari wa Bayern, Robert
Lewandowski, alipiga Bao 2 na Bao la 5 kufungwa na Mario Gotze, wote
hawa wakiwa Wachezaji wa zamani wa Dortmund.
Bao pekee la Dortmund lilifungwa na Mchezaji kutoka Afrika wa Nchi ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.
+++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Bayern 5
-Thomas Muller Dakika ya 26 & 35
-Robert Lewandowski 46 & 58
-Mario Gotze 66
Dortmund 1
-Pierre-Emerick Aubameyang Dakika ya 36
+++++++++++++++++++++++++++
Matokeo haya yameipaisha Bayern kileleni mwa Bundesliga
ikiwa na Pointi 25 kwa Mechi 8 wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili,
Dortmund.
VIKOSI:
Bayern Munich: Neuer; Lahm, Boateng, Martinez, Alaba; Alonso, Thiago; Muller, Gotze, Costa; Lewandowski
Akiba: Ulreich, Rafinha, Gaudino, Vidal, Coman, Kimmich, Steinhardt.
Borussia Dortmund: Burki; Piszczek, Hummels, Sokratis, Bender; Gündogan, Weigl; Mkhitaryan, Kagawa, Castro; Aubameyang
Akiba: Weidenfeller, Park, Hofmann, Januzaj, Reus, Ramos, Ginter.
BUNDESLIGA MATOKEO:
Darmstadt 2 FSV Mainz 3
Jumamosi Oktoba 3
Hertha Berlin 3 Hamburger SV 0
Hannover 1 SV Werder Bremen 0
TSG Hoffenheim 2 VfB Stuttgart 2
Borussia Monchengladbach 2 VfL Wolfsburg 0
FC Ingolstadt 2 Eintracht Frankfurt 0
Jumapili Oktoba 4
Schalke 04 0 FC Koln 3
Bayern Munich 5 BV Borussia Dortmund 1
Bayer 04 Leverkusen 1 FC Augsburg 1

Post a Comment