Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo mchana katika
uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo dhdi ya Malawi utakaocheza Jumatano
Oktoba 7, 2015 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Stars inayonolewa na kocha mkuu mzawa Charles Mkwasa, akisaidiwa na
Hemed Morroco, Peter Manyika na mshauri wa Ufundi Abdallah Kibadeni
wameingia kambini jana katika hoteli ya Urban Rose iliyopo Kisutu jijini
Dar es salaam.
Wachezaji wote wameripoti kambini isipokuwa wachezaji wa kimataifa
wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa, Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wanaotarajiwa kuungana na wenzao mwishoni mwa wiki
baada ya kumaliza michezo inayowakabili wikiendi hii.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa All Mustafa, Aishi Manula,
Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Haji
Mwinyi, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine ni viungo Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Said
Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva, Farid Musa,
washambuliaji John Bocco, Rashid Mandawa na Ibrahim Hajibu
STARS WAANZA KUJIFUA KUWAVAA MALAWI
Title: STARS WAANZA KUJIFUA KUWAVAA MALAWI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo mchana katika ...

Post a Comment