Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SILAHA 25 ZA ALGERIA DHIDI YA TANZANIA HADHARANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa Algeria, Christian Gourcuff ametangaza kikosi cha mwisho kinachotarajariwa kuivaa Tanzania kwenye mechi ya mchujo wa kuwan...


Kocha mkuu wa Algeria, Christian Gourcuff ametangaza kikosi cha mwisho kinachotarajariwa kuivaa Tanzania kwenye mechi ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu Kombe la Dunia  2018.Kikosi hicho kinajumuisha majina 25 ya wachezaji huku kipa Rais Mbolhi aliyedaka vyema kombe la Dunia akirejeshwa kikosini.
Nyota wa Dynamo Zaghreb, Soudan Hilal ameenguliwa kutokana na kuandamwa majeraha.
Mkali wa Valencia, Sofiane Feghouli  anayesumbuliwa na majeraha pia amejumuishwa katika kikosi hicho huku hali yake ikiendelea kuangaliwa kuelekea pambano la Jumamosi.
Taifa Stars ambayo imepiga kambi mchini Afrika Kusini kwa maandaalizi itamenyana na Algeria siku ya Jumamosi tar 14 mwezi huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana siku ya Jumanne mjini Algeirs.
Kikosi kamili:
Walinda Milango: Rais M’Bolhi (Antalyaspor / Uturuki), Azzedine Doukha (JS Kabylie), Malik Asselah (CR Belouizdad).

Viungo: Mehdi Zeffane (Rennes / Ufaransa), Mohamed Khoutir Ziti (JS Kabylie), Faouzi Ghoulam (Napoli / Italia), Djamel Mesbah (Sampdoria / Italia), Carl Medjani (Trabzonspor / Uturuki),Aïssa Mandi (Reims / Ufaransa), Hichem Belkaroui (Club Africain / Tunisia), Rami Bensebaini (Montpellier / Ufaransa).

Saphir Taïder (Bologna / Italia), Nabil Bentaleb (Tottenham / Uingereza), Walid Mesloub (Lorient / Ufaransa), Mehdi Abeid  (Panathinaikos / Ugiriki), Adelene Guedioura (Watford / Uingereza).
Sofiane Feghouli (Valencia / Hispania), Ryad Mahrez (Leicester / Uingereza) Yacine Brahimi (Porto / Ureno ), Ryad Boudebouz (Montpellier / Ufaransa), Said Benrahma (Nice / Ufaransa), Rachid Ghezzal (Lyon / Ufaransa)
Washambuliaji: Islam Slimani (Sporting / Ureno), Baghdad Bounedjah (ES Sahel / Tunisia), Ishak Belfodil (Bani Yas / United Arab Emirates).

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top