Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: LONDON DERBY: UNSTOPPABLE vs UNBEATEN
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
CHELSEA Arsenal na Liverpool ni timu pekee zilizofanikiwa kuifunga Chelsea. Kwa mazingira yale ya Chelsea kufungwa ilikuwa lazima lakini ta...

CHELSEA

Arsenal na Liverpool ni timu pekee zilizofanikiwa kuifunga Chelsea. Kwa mazingira yale ya Chelsea kufungwa ilikuwa lazima lakini tangu pale tumeshuhudia mabadiliko makubwa.

Chelsea imefanikiwa kushinda mechi 6 mfululizo tena bila kuruhusu goli kwenye nyavu zao. 3-4-3 ni mfumo ulioleta uwiano kwenye kikosi hiko kinachoongozwa na Conte.

Hazard amekuwa chachu ya maendeleo mazuri ya timu hiyo hivi karibuni. Ni mchezaji mwenye kasi na uwezo wa kufungua mabeki. Faida kubwa kwake kwa sasa ni kufunga magoli na kutengeneza pia.

Ubora wa Chelsea unaanzia kwenye safu ya ulinzi wao ambayo imekuwa ikicheza pamoja kwa muda mrefu huku wakipata msaada mkubwa kutoka kwa Kante ambaye amekuwa akishungulika na wapinzani kwenye kutibua mipango.

Tangu mfumo wa 3-4-3 uanze kutumika wing-back zao(Alonso na Moses) wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika kuleta uwiano wa kuzuia na kushambulia. Pia Diego Costa amekuwa kwenye ubora mzuri hususani katika kufunga magoli.

TOTTENHAM

Timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa kwenye ligi kuu England. Hapa mara nyingi amekuwa akitajwa Maurice Pochettino jinsi alivyoisuka timu hiyo tangu alipoichukua.

Ubora wa Spurs upo kwenye maeneo mengi ya kikosi chao kuanzia nyuma kwa mabeki,katikati kwa viungo, hadi mbele kwa washambuliaji.

Siku za karibuni kumekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye safu ya ulinzi baada ya Toby kupata majeruhi. Dier na Wimmer wamekuwa wakijumuisha kwa nyakati tofauti kusaidia na Vertonghen. Mabadiliko haya ya lazima yamekuwa yakiwagharimu mara kadhaa kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri.

Licha kuwa safu ya ulinzi ambayo haijakaa sawa msaada mkubwa wa timu hiyo unatoka kwenye safu ya ushambuliaji ambayo wamekuwa chachu ya ushindi licha ya kuruhusu magoli mara kadhaa.

Kurejea kwa Kane na Ali kumeongeza matumaini kwa Pochettino katika kufanya uchaguzi sahihi wa kikosi chake upande wa safu ya washambuliaji iliyojaa wachezaji wenye uwezo.

KEY BATTLE

Kama Rose na Walker watakuwa kwenye ubora wao wa kuzuia mapigo ya Alonso na Moses,Tottenham watakuwa na nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi dhidi ya Chelsea.

Kama Chelsea watakuwa kwenye ubora wao ule ule,safu ya ulinzi ya Spurs itakuwa kwenye matatizo makubwa na Chelsea watakuwa na sababu ya kuondoka na ushindi.

Kante dhidi ya Wanyama ni vita ya wanaume wawili ambao wameleta balance katika timu hizo. Atakaye kuwa nje ya uwezo wake ataipoteza timu yake.

Na: Ayoub Hinjo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top