Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: IJUE MIFUMO YA SOKA NA ILIPOTOKEA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mifumo ya soka inayotumika sasa imepitia historia ndefu sana ikibadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo makubwa katika " mbinu...

Mifumo ya soka inayotumika sasa imepitia historia ndefu sana ikibadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo makubwa katika " mbinu" na " ufundi " wa mchezo huu pendwa zaidi duniani.

Mfumo mama ambao umezaa mifumo yote inayotumika katika soka na iliyowahi kutumika na kuachwa ni 1-2-7 ambao ulitumika sana katikati ya 1800s lakini mwishoni mwa karne hiyo ( 19th ) ulifanyiwa marekebisho na kuzaliwa  2- 3 - 5.

Mfumo huu wa 2-3-5 ndio chanzo cha kuzaliwa kwa majina ya wachezaji na sehemu wanazo chezea uwanjani licha ya mengine kufutika baada ya marekebisho kadha wa kadha.

2-3-5 imetupa " full backs" katika eneo la ulinzi . Hapo unampata beki wa kulia( FR) na beki wa kushoto ( FL). Pia mfumo huu ukatupa left-half , centre half na right-half katika eneo la kiungo.

2-3-5 katika eneo la ushambuliajil ukatupatia out-side left ( left wing), inside left , centre forwad na out-side right ( right wing) .

Lakini baada ya ufahamu kuongezeka katika elimu ya soka hususani katika tacticts and techniques ( mbinu na ufundi) baadhi ya majina kama " half back " pale kati yaliondoka na kuanza kutumia majina kama midfield ( destroyer or defensive midfield) . Hii iliyokea sana miaka ya 1970s. Miaka ambayo mapinduzi makubwa katika mbinu , mifumo na aina ya uchezaji vilifanyika katika soka. Hiki ndicho kipindi dunia ilishuhudia wadachi wakiingia katika soka na patterns mpya za " total football". Uligeuka mfumo mama ulaya mashariki.

Total football ilikuja kukinzana na samba la kibrazil lililohasisiwa vyema na uboreshaji wa mfumo wa 4-2-4 na kuibuka kwa 4-3-3 lakini wazo likianzia kwa kwa waalimu wa Uruguayi ambao waliujaribu mfumo huo mwaka 1950 . Brazil waliingia na 4-3-3 kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia mwaka 1962 na kuonekana moto wa kuotea mbali. Mfumo unaoruhusu umilikaji mzuri wa mpira, kasi , kutawala eneo la kiungo, kushambulia pande zote na kuwalazimisha wapinzani muda wote kujilinda na kukosa muda wa kuwashambulia kutokana na pressing yenu. Brazil alinyakua ubingwa kwa kumtandika Czechoslovakia 3-1 mashindano yaliyofanyika nchini Chile akitumia mfumo huu . Mfumo ambao unaonekana kuwa sehemu ya utamaduni wa soka la kibrazili sambamba na 4-1-4-1 . Mifumo hii ndio inampa umaarufu mkubwa Tite kwa sasa ambaye ameiongoza Brazil the Selecao katika mechi nane bila kupoteza na kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwakani .

Asanteni
Samuel Samuel
02. 04. 2017

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top