1. Saimoni Msuva
Anasimama kama shujaa wa timu mpaka sasa. Amesaidia sana timu yake kwa ufungaji wa magoli mengi ndani ya timu pia kuwatengenezea wenzake nafasi za kufunga . Ana magoli 14 mpaka sasa pia akitoa assists 8! . Kwa mujibu wa benchi la ufundi ; ni mchezaji mwenye nidhamu na moyo wa kuitumika timu.
2. Haruna Niyonzima
Kama ilivyo kwa Saimoni Msuva yeye pia ameingia kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwaka. Kiungo huyu toka Rwanda hakuwa msaada sana mechi za awali mzunguko wa kwanza lakini mwishoni mwa raundi hiyo mechi za kanda ya ziwa na raundi hii , amegeuka mwiba mkali kwa wapinzani wa Yanga eneo la kiungo akisimama vyema na Thabani Kamusoko. Ndio passer namba moja ndani ya Yanga eneo kati .
3. Obrey Chirwa
Huyu hakupewa nafasi kabisa kuwika na klabu ya Yanga msimu huu . Akisajiliwa kwa gharama kubwa ndani ya klabu na kuvuta hisia kwa wapenzi wa timu hiyo na wadau wa soka nchini, alishindwa kuwa bora mzunguko wa kwanza lakini ana maliza ligi akiwa na goli 12 ligi kuu na 5 FA na kusimama kama moto wa kuotea mbali katika upachikaji magoli.
4. Hassani Kessy
Migogoro ya kesi ya kimkataba na Simba SC kuja Yanga haikumpa saikolojia nzuri mwanzoni mwa msimu. Mzunguko wa pili amegeuka mchezaji tegemeo kikosi cha kwanza. Kuumia kwa Juma Abdul kulimpa namba ya kudumu kikosini pia hata baada ya kupona bado analeta changamoto chanya.
5. Beno Kakolanya
Mlinda mlango huyu ukiwa ni msimu wake wa kwanza na Yanga SC akitokea Prisons, amekuwa bora kila akipewa nafasi langoni na kutishia kabisa utawala wa Munishi katika milingoti ya Yanga SC. Amekuwa bora na makini sana .
6. Vicente Bossou
Ni muhimili imara wa Yanga SC katika safu ya ulinzi . Uzoefu wake unamfanya kutengeneza kombinesheni nzuri na wenzake watatu Nadir , Chikupe ba Yondani . Hajapata mechi nyingi kutokana na umajerihi na uwakilishi wa nchi yake ya Togo kwenye michuano ya AFCON mwaka huu.
7. Geofrey Mwashuiya
Baada ya kuumia mwanzoni mwa msimu na kukaa nje ya uwanja kwa wiki 8 alionekana kukatiwa tamaa na wapenzi wa timu hiyo na ukizingatia hapo mwanzo hakuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi. Mzunguko wa pili wa ligi amekuwa vyema na kuaminika na benchi la ufundi kuanza kikosi cha kwanza . Anaingia katika orodha hii kama chipukizi anaekuja vyema katika soka . Kuna vitu akipunguza mfano chenga na ukokotaji usiokuwa na faida , atafika mbali kama winga wa kushoto wa timu hiyo .
8. Thabani Kamusoko
Kama sio kuwa majeruhi mara kwa mara basi angeibuka tena mchezaji bora wa kulipwa ligi kuu. Licha ya usajili wa Justine Zulu kama kiungo mkabaji msimu huu, Kamusoko anageuka shujaa eneo la kiungo cha chini cha Yanga SC . Ndio box to box midfielder wa kuaminiwa ndani ya klabu hiyo kwa sasa . Nidhamu na utulivu ni faida nyingine kwake.
9. Haji Mwiji
Huyu ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi ndani ya timu hiyo msimu huu . Mpaka sasa ameichezea Yanga SC mechi 21! . Ndio beki wa kutumainiwa wa timu hiyo upande wa kushoto .
10. Juma Abdul
Huyu aliibuka mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita. Msimu huu ameuanza vibaya kwa majeruhi lakini anaimalizia ligi akiwa moto kali na kuonesha kupaji halisi kama beki wa kulia . Ana uwezo mzuri kwenye marking na kupandisha mashambulizi kwa kupiga krosi zenye macho.
11. Deogratius Munishi
Amedaka mechi nyingi kuliko kipa yoyote yule ndani ya Yanga . Uzoefu na uwezo wake unamfanya kusimama kama golikipa namba moja ndani ya Yanga .
12. Amisi Tambwe
Msimu uliopita wakisimama mbele pamoja na Donald Ngoma walikuwa ni moto wa kuotea mbali wakifunga zaidi ya goli 30 wao wawili. Majeruhi ya muda mrefu yeye na Ngoma msimu huu yamemfanya kutokufunga goli nyingi . Mechi hizi za mwisho Tambwe amerudi kwenye ubora wake na kuifungia magoli muhimu timu yake.
13. Emanuel Martin
Ingizo jipya msimu huu . Amechukua muda mfupi kuizoea falsafa ya Yanga SC kushambulia kwa kasi kupitia kwenye wings . Mechi na Toto Africa huyu ndio alikuja kugeuza matokeo kwa pressing zake . Naiona future nzuri juu yake .
14. Kelvin Yondani
Amekuwa bora kwa kipindi kirefu . Ukimwindoa Bossou kwenye safu ya ulinzi , Yondani anasimama kama sweeper makini ingawa msimu huu hajawa bora sana kama misimu mitatu ya nyuma lakini bado ni tegemeo katika klabu ya Yanga . Kuanza kumtumia kama kiungo wa chini iliongeza credit kwake lakini bado ana tatizo la asili la matumizu ya nguvu sana yanayompa kadi mara kwa mara na kuonekana mtovu wa nidhamu sometimes.
Note: Orodha hii haijapangwa kutokana na ubora wa mchezaji.
Samuel Samuel
18.05.2017
Post a Comment