Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: HAKUNA WAKUMZUIA CHIRWA KUWA MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Obrey Chirwa alipowasili ndani ya Yanga SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Platinum alionekana kushindwa kuendana na kasi ya timu pia mfu...

Obrey Chirwa alipowasili ndani ya Yanga SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Platinum alionekana kushindwa kuendana na kasi ya timu pia mfumo wa ligi yetu ambao ni tofauti sana na Zimbabwe alipokuwa akicheza .

Hans Van Pluijm aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga SC ambaye ndie aliyemsajili mshambuliaji huyo tokea FC Platinum hakukata tamaa juu yake na kila mara kumpa nafasi ili aweze kuzoeana na wenzake pia kuizoea ligi ya Tanzania.

Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu ulikuwa mgumu sana kwake mchezaji huyo ambaye alisajiliwa dirisha dogo la usajili kombe la Shirikisho Afrika 2016 . Ugumu mkubwa ulitokana na kombinesheni ya muda mrefu ya Amisi Tambwe na Donald Ngoma ambao walitawala vyema safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara.

Kushindwa kung'ara kwa mshambuliaji huyo kulianza kuwapa wasi wasi wanachama wandamizi wa klabu hiyo akiwepo kiongozi wa baraza la wazee ndani ya Yanga SC mzee Akilimali ambaye alikiri Yanga SC kuingizwa chaka kwa mchezaji huyo na kutamka bila woga kwenye vyombo vya habari ' Chirwa galasa '.

Mabadiliko ya benchi la ufundi la Yanga SC kwa kuondoka mdachi Hans Van Pluijm na kuingia mzambia George Lwandamina, ilikuwa ni taa ya kijani kwa mshambuliaji huyo toka Zambia.

Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Obrey Chirwa alimaliza akiwa na magoli matatu tu ! lakini mzunguko huu akitumiwa kama mshambuliaji wa kati  amefikisha magoli 12! kwenye ligi kuu tofauti ya goli 2 na Saimoni Msuva mwenye goli 14 kileleni mwa msimamo wa wafungaji wa ligi kuu. Kasi na uwezo huu vimechangiwa na Lwandamina kumpa nafasi mara kwa mara na imechangiwa sana na kuumia kwa wote wawili Ngoma na Tambwe kwa vipindi tofauti. Lakini kikubwa ni uwezo wa benchi la ufundi kuutengeneza mfumo wa kushambulia wa timu hiyo kumzunguka yeye.

Sambamba na magoli 12 ya ligi kuu , Chirwa pia mpaka sasa ndio mfungaji bora wa kombe la ASFC akiwa na magoli 5 na kumfanya awe na magoli 17 katika ligi zote mbili.

Mabadiliko haya yamejibu maswali na kejeli zote juu yake na kuwapa somo watanzania kuwa na kiasi katika kutoa shutuma juu ya mchezaji wakati bado hajapewa muda wa kutosha kuonesha alichonacho.

Wiki ijayo zinatoka Tuzo za msimu wa 2016-2017 mpaka sasa sijaona wakumfanya Chirwa kubeba tuzo hiyo kwani kwa muda mfupi aliotumikia Yanga ameweza kufanya makubwa.
Tuzo iyo ambayo msimu uliopita aliichukuwa Mzimbabwe Thaban Scala Kamusoko.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top