Ikiwa ni siku ya tatu baada ya serikali kupitia wazi michezo na utamaduni mh.Nape Nauye kuzifungia Timu za Yanga na Simba kutumia uwanja wa taifa.
Klabu bingwa Tanzania bara Young africans sports club leo hii imeamua kuiandikia barua wizara husika na kuhusu wapi watapatumia kwenye mechi zao.
Kaimu katibu mkuu wa Yanga leo hii ameandika barua kwenda wizarani ikiwa inautambulisha uwanja wa Amani Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani kwa mashindano yake yote ambayo timu ya Yanga inashiriki mpaka pale uwanja wa taifa utakapoanza tumika kwa vilabu ivyo vya Simba na Yanga.
Hivyo Yanga wao wapo tayari kwenda zanzibar na wanachokisubiri ni majibu toka wizarani juu ya ombi lao hilo kwani wao kama Yanga tayari kila kitu kipo sawa juu ya kutumia uwanja huo wa Amani Zanzibar.


Post a Comment