Kipenzi cha wanajangwani , kocha mwanachama pia waweza muita kocha bora wa ligi kuu Tanzania bora msimu wa 2015-16 Hans Van Pluijm leo tarehe 28 Octoba ametengua uamuzi wake wa kujiuzulu kuifundisha Yanga SC.
Hans Van Pluijm alijiuzulu kuifundisha timu hiyo tarehe 25 Octoba baada ya kutua jijini Dar es salaam akitokea Kagera alipoiongoza timu yake kuifanyia dhahama ya mwaka Kagera Sugar kwa ushindi wa goli 6-2.
Hans Van alijiuzulu kutokana na sababu binafsi msingi mkubwa ukiwa ni kusimamia heshima na stahiki zake ndani ya klabu hiyo pendwa.
Uongozi wa Yanga unayofuraha kubwa kuwataarifu wapenzi , wanachama , mashabiki na wadau wa michezo nchini kwamba, klabu kwa kutambua umuhimu , rekodi na mbinu za mwalimu huyu uliamua kukaa nae chini na kumsihi kutengua uamuzi wake jambo ambalo limefanikiwa.
Kufanikiwa huku kumetokana na mapenzi mazito ya mwalimu huyu kwa klabu hii.
Hans Van Pluijm mwenye mkataba wa miaka miwili na Yanga SC anarudi kama mkurugenzi wa ufundi.
Tunachukua fursa hii kuwaomba wapenzi , wanachama na mashabiki wa klabu hii kuendeleza umoja wa asili wa wanajangwani ili klabu ifikie malengo yake ya kutetea ubingwa.
Hapa mnatuchanganya maana inasemekana tayar mzambia na yeye alishasaini mkataba.
ReplyDeleteITAKUWAJE?
Your blog is very useful for me.I really like you post.Thanks for sharing.
ReplyDeleteดูหนัง