Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: DONALD NGOMA AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUTOA LA MOYONI KUONDOKA KWA HANS VAN PLUIJM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji mahiri wa Yanga SC toka nchini Zimbabwe Donald Dombo Ngoma , ameshitushwa sana na kujiuzulu kwa kocha mkuu wa klabu hiyo ndugu ...

Mshambuliaji mahiri wa Yanga SC toka nchini Zimbabwe Donald Dombo Ngoma , ameshitushwa sana na kujiuzulu kwa kocha mkuu wa klabu hiyo ndugu Hans Van Pluijm.

Leo asubuhi viwanja vya polisi wakati kocha huyo alipohudhuria mazoezi ya timu kwa mara ya mwisho ikiwa ni kuja kuwapa mkono wa kwaheri vijana, Ngoma alionesha huzuni sana na muda wote alikuwa kimya.

Huzuni ya mchezaji huyo ambaye Hans Van Pluijm alimsajili toka FC Platinum msimu wa 2015-16 imeonekana dhahiri kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Ngoma kaandika maneno haya " Goodluck in the next life big man Hans Van Pluijm . Coach had me in so many events I got confused"

Tafsiri isiyo rasmi " maisha mema uendako mwalimu Hans Van Pluijm. Umenipitisha kwenye matukio mengi nilipo sasa nimechanganyikiwa"

Donald Ngoma sambamba na mwenzake Thabani Kamusoko ni moja ya usajili makini uliyowahi kufanywa na kocha Hans Van Pluijm. Donald Ngoma alimtengenezea kombinesheni nzuri na Amisi Tambwe na muunganiko huo kuipa Yanga goli 30 msimu uliopita kwa wao wawili tu . Ngoma akifunga magoli 9 na Tambwe goli 21 lakini Ngoma akisimama kama mchezeshaji wa mwisho eneo la ushambuliaji pia daraja kimbinu kwa viungo wa kati na safu ya ushambuliaji.

Ngoma ana kila sababu ya kumkumbuka kocha huyo ambaye katika mechi 30 za ligi kuu alimpa mechi 25 acheze ikiwa ni fursa kuonesha kipaji chake na wanajangwani kumuelewa pia wadau wengine wa michezo.

Lakini mwalimu Hans Van Pluijm amewaasa wachezaji kutoweka vichwani jambo lake la kujiuzulu zaidi kumpa ushirikiano mwalimu msaidizi Juma Mwambusi aliyebaki na timu na kocha yoyote ajae.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top