Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: ZESCO UNITED SC WATOA TAMKO JUU YA KOCHA WAO GEORGE LWANDAMINA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa timu ya soka ya Zesco United umetoa tamko kufuatia taarifa za vyombo vya habari nchini humo kutoa taarifa za kocha wao mkuu ndug...


Uongozi wa timu ya soka ya Zesco United umetoa tamko kufuatia taarifa za vyombo vya habari nchini humo kutoa taarifa za kocha wao mkuu ndugu George Lwandamina kutimkia Tanzania kufanya mazungumzo na klabu ya Yanga SC kwa ajili ya kujiunga nao.

Uongozi umesema wanachotambua wana mkataba na kocha huyo wa miaka mitatu unaokwisha January 17 mwakani.

Uongozi wa Zesco kwenye taarifa yao kwa vyombo vya habari wanasema wamekuwa wakimshawishi kocha huyo kuongeza mkataba na klabu yao lakini amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha hivyo taarifa za kocha huyo kuwa Tanzania zimekuwa za ghafla kwao na uongozi hauna taarifa za kocha huyo kuwa nje ya nchi.

Uongozi wa Zesco United unachotambua kocha huyo aliomba ruksa kwenda kwao kuhudhuria msiba wa familia na ruksa alipata toka kwa meneja wa timu ndugu Mabvuto Banda.

George Lwandamina alitarajiwa kurudi jana ( 24 Octoba ) kwa ajili ya kuiandaa timu na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Nkwazi FC jijini Lusaka.

Uongozi wa Zesco unatanabaisha kama taarifa za kocha huyo zakuwa Tanzania kufanya mazungumzo na Yanga SC ni za kweli, basi klabu hiyo inategemea kocha huyo atakuwa muungwana kwa kuwapa taarifa na kuvunja mkataba wake ingawa watasikitishwa na utaratibu ulivyokwenda.

Uongozi wa Zesco unazidi kumkumbusha mwalimu huyo kukumbuka vyema vipengele vya mkataba wao endapo upande mmoja utahitaji kuvunja mkataba.

Taarifa hii kwa vyombo vya habari nchini Zambia imetolewa na Richard Mulenga na Katebe Chengo kaimu katibu mkuu na afisa habari wa klabu ya Zesco United.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top