Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .
Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.
Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .
Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tafadhali usifnye hivyo maana yanga itapotea kimpira kwa ajili y wapuuzi wachache
ReplyDeleteHabari yenyewe haina uhakika kwa mfano mtu anasema endapo Manji atajitoa, huku akisema habari za uhakika wapi na na wapi
ReplyDeleteManji endelea kubaki yanga kwa maendeleo ya timu yetu
ReplyDeleteTunakuhtaji tafadhal
ReplyDeleteAfadhal hata ulivyochukua uamuz huo manji achana nao hao vyura fc
ReplyDeleteAfadhal hata ulivyochukua uamuz huo manji achana nao hao vyura fc
ReplyDeleteVery nice post.really I apperciate your blog.Thanks for sharing.keep sharing more blogs.
ReplyDeleteดูหนัง