Nahodha wa timu ya taifa ya Brazil mwaka 1970 ikichukua kombe dhidi ya Italia , amefariki leo na kuamsha simanzi kubwa katika taifa hilo kubwa Amerika ya kusini.
Carlos Albero yupo katika rekodi ya walinzi bora wa muda wote kuwahi kutokea katika kikosi cha Brazilli. Amefariki leo Octoba 25 akiwa na miaka 72! kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Mwaka 1970 akiwa nahodha wa Brazil alifunga goli la nne kwenye fainali likihesabika ni goli bora kabisa kuwahi kufungwa kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia . Zilipigwa pasi tisa tu na wachezaji 9 wa Brazil na yeye akiwa wa mwisho aliachia mkwaju mzuri na kutinga nyavuni.
Kabla ya kifo chake cha ghafla alikuwa mtangazi wa kituo maarufu cha runinga jijini Reo de Janeiro kama mchambuzi wa masuala ya soka na habari za michezo . Kituo kinaitwa Spor Tv. Mara ya mwisho kuonekana kazini ni siku mbili zilizopita kabla mauti hayajamfika.
Mwaka 2003 serikali ya Brazil iliruhusu jina lake kuingia katika kumbukumbu za kitaifa katika rekodi za Brazilian Hall of Fame.
2004 Shirikisho la soka duniani FIFA lilimjumuisha katika orodha ya wacheza 100 bora wa muda wote duniani wanao ishi .
Huyu ndio Albero Carlos gwiji la klabu ya Santos aliyoichezea mechi 445 na kufunga magoli 40 akisimama kama mlinzi wa kushoto.
Samuel Samuel
Post a Comment