Mshambuliaji mwenye uraia wa Zambia akitokea FC Platinum ya nchini Zimbabwe na kujiunga na Yanga SC msimu huu , ametumia dakika 345 kuipa Yanga SC magoli matano mpaka sasa.
Obrey Chirwa mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo mshambuliaji, mshambuliaji wa kati na winga kulia au kushoto, alianza kwa kusuasua ndani ya klabu hiyo yenye masikani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar hali iliyowafanya wapenzi wa timu hiyo na wadau wa soka nchini kuanza kumkatia tamaa.
Chirwa aliyejiunga na Yanga SC dirisha dogo la usajili kombe la shirikisho , aliweza kucheza mechi zote za shirikisho bila kutikisa nyavu mwalimu Hans Van akimpanga kama kiungo mshambuliaji au mshambuliaji wa kati sanjari na Donald Ngoma.
Makali ya mzambia huyu yamesubiri ufunguzi wa ligi kuu nchini ndipo yajidhihirishe ndani ya dakika 345.
Yanga SC ikicheza mechi ya saba katika ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda 3-1 ndipo Chirwa alipopata nafasi ya kufunga goli la tatu. Magoli mengine yakifungwa na Simoni Msuva akifunga goli la kwanza na goli la pili Donald Ngoma.
Mechi ya tisa dhidi ya Toto Afrika jijini Mwanza Chirwa alitikisa nyavu goli la pili akitanguliwa na Simoni Msuva aliyefunga goli la kwanza.
Ndani ya Kaitaba mkoani Kagera mechi namba 93 kwenye ratiba ya TFF dhidi ya Kagera Sugar alifunga goli la sita kuhitimisha karamu ya ushindi mkubwa zaidi ndani ya ligi kuu wa 6-2.
Mzambia huyu aliendelea kuwathibitishia watanzania ubora wake jana katika mchezo dhidi ya Ruvu JKT akifunga goli lake la tano katika ligi akipishana goli 2 tu na kinara wa ufungaji Shiza Kichuya wa Simba SC mwenye goli 7.
Kutimiza dakika 345, Chirwa alicheza dakika 90 dhidi ya Ndanda FC, akacheza tena dakika 90 dhidi ya Mtibwa Sugar kujipa dakika 180 kuitumikia Yanga ndani ya ligi kuu.
Alipata nafasi ya dakika zingine 90 dhidi ya Toto Afrika na kujiweka rekodi ya kucheza dakika 270. Mechi dhidi ya Kagera Sugar alitolewa dakika ya 75 akiweka mtaji wa dakika 345 kuitumikia Yanga kabla ya jana kuhitimisha rekodi ya dakika 435 akiwa na goli 5. Ni rekodi nzuri kwa wastani wa mechi 5 katika ligi.
Post a Comment