Beki wa zamani wa Manchester United Garry Neville anaona bora timu ya Manchester United iuzwe na ufanyike uwekezaji mpya ndiyo klabu hivyo itakuwa sawa.
Garry Neville 🗣️
"Wamiliki wa klabu ya Manchester United ambao ni familia ya Glazer wanatakiwa waiuze hii klabu nafikiri itakua na maendeleo zaidi".
"Labda uwekezaji mpya ukifanyika kwa watu tufauti unaweza ukawa na faida kwa hii klabu".
"Timu ina muda mrefu sana haipati matokeo haina muonekano wa kuwania taji lolote kwenye msimu".
"Wachezaji wanasambaratika tu hats uwanja wa mazoezi unaonekana kama hauna faida".
"Manchester United imekua ni timu ya kati ambayo malengo yake ni kupambana isishuke daraja tu wakati hii ilikua ni klabu kubwa duniani na sio tu Uingereza".
" Timu imepoteza malengo kuna muda unaona kabisa hii sio hadhi ya Manchester United".
Post a Comment