- Historia ya klabu ya Yanga inaanzia mwaka (1910) ingawaje rasmi klabu hiyo ilisajiliwa February 11, 1935.
- Yanga ndio klabu ya kwanza kuanzishwa East Africa, ilianzishwa na waasisi kwa dhumuni kuu la kusaidia katika harakati za UKOM OZI / Kudai uhuru wa Tanzania na nchi zingine za Africa.
- Wakati huo ilikuwa hairuhusiwi wazalendo (Weusi) kukusanyika ovyo hapo ndipo lilipotokea wazo la kuianzisha klabu hii kwani kupitia yenyewe ingesaidia kuwakutanisha vijana wapigania uhuru kupanga njia za kudai uhuru.
- Mnamo mwaka (1936) ulitokea mgogoro baina ya viongozi wa Yanga, baadhi ya viongozi wachache wenye asili ya Asia walijitoa na kwenda kuanzisha timu nyingine iitwayo QUEEN FC. Baadae QUEEN FC ilibadili jini na kujiita Sunderland.
📌 Baada ya Uhuru (1963) Makao makuu ya Yanga yalikuwa bado yako kwenye nyumba ya kupanga,, Mwenyekiti wa Yanga wa wakati huo Mohammed Sultan (Mabosti), Mzee Kitwana Kondo makamu Mwenyekiti na mzee Jabir Katundu katibu mkuu wa Yanga enzi hizo, walikuja na wazo la Yanga kumiliki Jengo lake.
- Mwaka (1964) viongozi hao wa Yanga waliandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya ABALUHYA 🇰🇪 ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka huo.
- Katika mchezo huo Yanga ilifanikiwa kupata pesa nyingi kiasi cha Tsh Elfu (13), Pesa hizo ndizo walizokwenda kununua jengo la MAFIA ambalo mpaka leo lipo mtaa wa Mafia Nyamwezi, hivyo kuwa klabu ya kwanza East Africa kumiliki jengo lake.
- Mwaka (1969) viongozi wa Yanga waliona kuwa Yanga inahitaji kuwa na makao makuu na jengo lenye hadhi zaidi kuliko lile walilokuwa nalo la Mafia, hivyo wakafunga safari hadi kwa mwanachama wa klabu hiyo Hayati Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar kumuomba ufadhili.
📌 Raisi Karume alikubali wazo hili ila akawapa sharti moja, lazima viongozi hao wa Yanga waje na viongozi wa Sunderland (Simba SC) ndipo atatekeleza ombi hilo. Viongozi wa Yanga wakawafuata viongozi wa Sunderland.
- Hayati Karume alikubali kujenga jengo moja ambalo litamilikiwa na klabu zote mbili Yanga na Sunderland,, Wazo hilo liligonga mwamba kutokana na upinzani waliokuwa nao.
- Hayati Karume kupitia kwa mzee Rashidi Kawawa aliwakabidhi mzee MANGALA na mzee MWINYIKAMBI hundi yenye thamani ya Tsh milioni 2 waende wakaanze ujenzi wa jengo la Yanga sc na pia akawapa viongozi wa Sunderland kiasi pubgufu kidogo ya hicho wakajenge pia jengo lao.
- Viongozi wa Yanga kwa kushirikiana na Wajerumani walipata mchoro na mkandarasi wa kujenga jengo kwa Tsh laki 8,, Wakapeleka mchoro city Council kwa ajili ya kuthibitishwa.
📌 Walipofika city council, Engineer mmoja aliyejulikana kwa jina la LUNYASI ambaye pia alikuwa mwanachama wa Sunderland alikataa kupitisha mchoro huo kwa madai kuwa eneo lile ni jalala, likijengwa jengo litaanguka.
- Viongozi wa Yanga walifunga safari hadi kwa Hayati Karume na kufikisha taarifa hiyo,, Hayati Karume bila kusubiri akaondokas moja kwa moja mpaka JANGWANI Kariakoo, akaweka jiwe la msingi ambalo liko mpaka leo hapo makao makuu ya Yanga na kuruhusu ujenzi uanze mara moja.
- Baadae klabu ya Sunderland ikabadili tena jina baada ya marehemu Kawawa kuitaka kubadili jina la kikoloni na kujiita jina lingine,, Viongozi wa Sunderland wakabadili jina na kujiita SIMBA SC.
NB ; Jengo la Yanga likakamilika na jengo la Simba likakamili. Majengo hayo yapo mpaka leo,, Yote mawili yalijengwa kwa pesa aliyotoa Hayati Karume 🙌
📌 Tangu mwaka (1935) mpaka sasa klabu ya Yanga ndio klabu iliyokusanya makombe mengi zaidi East Africa na haya ni baadhi ;
🏆 27 = Ligi kuu Tanzania bara.
🏆 07 = Kombe la Pall Mall.
🏆 06 = Ligi ya muungano.
🏆 06 = Ngao ya jamii
🏆 05 = CECAFA Kagame cup.
🏆 04 = Kombe la Majimbo.
🏆 03 = Kombe la Nyerere.
🏆 03 = Kombe la FAT.
🏆 02 = Kombe la Mapinduzi.
🏆 02 = Kombe la Tusker.
🏆 02 = Kombe la Songambele.
🏆 02 = Kombe la Afro Shiraz.
🏆 01 = Kombe la Healthlo
🏆 01 = Kombe la Maendeleo.
🏆 01 = Kombe la Kassum.
🏆 01 = Kombe la TAA.
🏆 01 = Kombe la Hedex.
🏆 01 = Kombe la Mei mosi.
🏆 01 = Kombe la Ukombozi.
🏆 01 = Kombe la (FA)
🏆 Nk...............
🎂 Happy birthday Young Africans 🙌
Post a Comment