F
IFA imethibitisha kuwa inachunguza Uhamisho wa Eliaquim
Mangala kutoka FC Porto kwenda Manchester City kutokana na kukiukwa kwa
Sheria zinazokataza Mchezaji kumilikiwa na pande tatu.
Mangala, Mchezaji wa Kimataifa wa France, ameichezea Man
City mara 31 kwenye Ligi Kuu England tangu ahamie hapo kutoka Porto
Agosti 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 32.
Imedaiwa kuwa Kampuni iitwayo Doyen Sports, yenye Ofisi
zake Nchini Malta na Jijini London, ililipa Pauni Milioni 2 Mwaka 2011
ili kununua Hisa za Umiliki wa Mchezaji huyo wakitegenea thamani yake
itapanda.
Inasemekana baada ya City kumnunua Mangala kutoka Porto,
Doyen Sports ililipwa Pauni Milioni 10.6 kama mgao wao wa mauzo ya
Mchezaji huyo.
Ikiwa uchunguzi wa FIFA utabaini kuna ukiukwaji wa Sheria
basi FC Porto, na si Man City, ndio watakaoadhibiwa kwa kupigwa Faini au
kufungiwa Kuuza au Kununua Wachezaji.
Mangala alianza Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Klabu ya
Belgium Namur na kisha kuchukuliwa na Standard Liege akiwa na Miaka 17
ambako alicheza Mechi Zaidi ya 100 kwa Timu ya kwanza na kisha kujiunga
na Porto.


Post a Comment