Ndugu wanachama,
mashabiki wa Simba na Watanzania wenzangu, Nchi yetu tuipendayo ya Tanzania
inafanya uchaguzi tarehe 25 Oktoba 2015.
Kwa niaba ya Uongozi wa Simba tunapenda kuwatakia Watanzania
wote Uchaguzi mwema. Amani, ni tunu tuliyopewa na Mungu na pia Waasisi wa Taifa
hili, hivyo ni jambo la muhimu mno kuitunza na kuienzi.
Amani na Umoja ndio msingi muhimu wa maendeleo sio tu wa kiuchumi
bali pia mpira wa miguu.
Napenda kumalizia kwa kuwashukuru kwa kuendelea kuishangilia
timu yenu.
Evans Aveva
Rais wa Simba

Post a Comment