Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi kati ya Yanga SC dhidi ya
Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
kiingilio vha chini kikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vyenye
rangi ya bluu, Kijani na Machungwa.
Tiketi za mchezo huo zitauzwa siku ya mchezo Jumamosi katika eneo la
Uwanaj wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo kingilio cha juu kitakua ni
Shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, na Shilingi Elfu Ishirini
(20,000) kwa VIP B & C.
Mwamuzi wa mchezo huo atakua Abdallah Kambuzi kutoka mkoani
Shinyanga, akisaidiwa na Makame Mdogo (Shinyanga), Robert Luhemeja
(Mara), mwamuzi wa akiba Frank Komba (Dsm) huku Kamisaa wa mchezo akiwa
Joseph Mapunda kutoka mkoa wa Ruvuma.
KUWAONA YANGA NA AZAM BUKU TANO TU
Title: KUWAONA YANGA NA AZAM BUKU TANO TU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi kati ya Yanga SC dhidi...

Post a Comment