Katika kuimarisha maandalizi ya
Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi
mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi
ameunda kamati maalum itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake
yatakua:
(i) Kuimarisha huduma kwa
wachezaji,
(ii) Uhamasishaji na Masoko,
(iii) Kuhamasisha wachezaji,
(iv) Kuandaa na kusimamia mkakati
wa Ushindi.
Kamati hii itaongozwa na Mwenyekiti
Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael
Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la
kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu
hayo.
Wadau wa mpira wa miguu ambao
kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika
kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.
Post a Comment