Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’,
Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na
michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba
21, nchini Ethiopia.
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema
wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi
na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata
nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
“Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na
wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini
tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani
Afrika” amesema Kibadeni.
Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi
Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe
(Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka
(Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani
(Yanga).
Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba),
Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga),
washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim
Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa
kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka,
Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam
chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji
wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.
Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku
kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa
wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.
KING KIBADENI ATANGAZA KIKOSI CHA CHALLENJI
Title: KING KIBADENI ATANGAZA KIKOSI CHA CHALLENJI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na mich...

Post a Comment