Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kitafanya mazoezi leo jioni saa 1
Algeria, sawa na saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja
wa Mustapher Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji
Algeria.
Stars inayonolewa na kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa
iliwasili salama jana jioni katika mji wa Blida, uliopo takribani
kilometa 75 kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari
Boumediene jijini Algiers.
Mkwasa amesema mchezo wa kesho watajituma kadri ya uwezo kuhakikisha
wanapata ushindi, makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali
yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watapambana kusaka ushindi
katika mchezo huo.
Wachezaji wote 21 wapo katika hali nzuri, hakuna mchezaj majeruhi
hata mmoja, hivyo kocha Mkwasa ana wigo mpana wa kumtumia mchezaji
yoyote anayemuhitaji kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka
2018, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Mali na utaanza saa 1:15
usiku (Algeria) sawa na saa 3:15 usiku kwa saa nyumbani Tanzania na
Afrika Mashariki.
STARS KUWAVAA ALGERIA KESHO
Title: STARS KUWAVAA ALGERIA KESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kitafanya mazoezi leo jioni saa ...

Post a Comment