Uganda,
wakicheza nyumbani katika uwanja wa Mandela waliifunga Togo 3-0 na hivyo wakawa
wameshinda kwa jumla ya mabao 4-0 ambapo mchezo wa kwanza walishinda kwa bao
1-0.
Gabon nao
wakasonga mbele katika hatua ya makundi kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3
dhidi ya Msumbiji.
Nao Zambia,
wakawachapa Sudan kwa 2-0 na kufuzu kwa makundi kwa jumla ya mabao 3-0 huku
mabao ya jana yakifungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo.
DR Congo
walitoka sare ya 2-2 na Burundi huko kwao lakini wamesonga mbele baada ya kushinda
mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko Bujumbura.
Morocco nao
wamefuzu licha ya kufungwa 1-0 jana na Equatorial Guinea baada ya wao kushinda
mechi ya kwanza 2-0.
Timu hizi 6
zilizofuzu zitaungana na nchi nyingine 14 zitakazofuzu Jumanne na kupangiwa makundi
matano ya timu 4 kila kundi.
Mshindi
mmoja wa kila kundi atafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko
Urusi.

Post a Comment