Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria leo
jioni majira yaa 10 jioni, kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mji
wa Bilda.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,
Athumani Kambi, ambapo jumla ya watu 40 wapo katika mji wa Bilda
wakiwemo wachezaji 21 wanaojiandaa kwa mchezo wa marudiano.
Mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege Algiers, Stars
ilipokelewa na watanzania na wanafunzi wanaoshi nchini Algeria, na
kuongozana na timu mpaka katika mji wa Bilda ilipofiki timu.
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho saa 1 jioni katika uwanja wa
Mustapha Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa marudiano siku ya Jumanne.
Katika mchezo wa awali uliochezwa jana jioni jijini Dar es salaam,
Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Algeria, hivyo kuifanya
Stars kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano ili kuweza kusonga
mbele.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vjana wake wote wapo
katik ahali, hakuna majeruhi na wapo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi
siku ya Jumanne, na kusema makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana
wanayafanyia kazi yasijitokeze tena katika mchezo unaofuata.
Taifa Stars imefikia katika hoteli ya Ville Des Roses imetumia
takriabn muda wa saa 1 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Algiers mpaka
katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Bilda.
STARS YAWASILI SALAMA ALGERIA
Title: STARS YAWASILI SALAMA ALGERIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria le...

Post a Comment