Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: STARS YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza  na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya ta...
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza  na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.
Elius Maguli alianza kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 43 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi. Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili stars ilanza kwa kupata goli la pili kocha alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Elius Maguli na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya.

Stars ilijikuta ikifungwa magoli mawili ya haraka kabisa ambayo yameifanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 2-2 matokeo ambayo yanawafanya Stars sasa kuhitaji ushindi au sare ya zaidi ya magoli zaidi ya matatu ili kuvuka.

Mechi ya marudiano itapigwa katikati ya wiki hii na mshindi ataingia katika makundi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top