Klabu hiyo pia iko mbioni kuvunja
rekodi ya kuvuka Mapato ya pauni milioni 500 na kuweka Rekodi ambayo hajafikiwa
na Klabu yeyote.
Mapato ya Man United kwa Miezi
Mitatu, iliyoiishia Septemba, ni Pauni Milioni 123.6 ikiwa ni ongezeko la
Asilimia 39 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka 2014.
Pia mapato yameongezeka baada ya
kusaini Mkataba mpya na kampuni ya vifaa vya michezo vya Adidas ambayo
yatawaingizia Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10 ukiwa ni Mkataba mkubwa kabisa
Duniani kwa Klabu na Watengeneza Vifaa vya Michezo.
Vilevile, kushiriki kwa timu hiyo
katika michuano ya Uefa Championz ligi kumechangia ongezeko la pato lao kwenye
Matangazo ya Mechi kwa Asilimia 64.3.
Asilimia 64.2 hutokana na
vingilio vya mashabiki pamoja na kuuzwa kwa bidhaa nyingine zikiwemo jezi.


Post a Comment