Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: KPAH SHERMAN ATUA CYPRUS
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
na Samuel Samuel Mliberia aliyepita Yanga SC baada kuuzwa Mpumalanga nchini Afrika Kusini na kwenda kwa mkopo Santos , sasa ametua katika k...

na Samuel Samuel
Mliberia aliyepita Yanga SC baada kuuzwa Mpumalanga nchini Afrika Kusini na kwenda kwa mkopo Santos , sasa ametua katika klabu ya Dumlupnar Turk SP .

Kpah ana uwezo mzuri wa kumiliki mpira katika safu ya ushambuliaji na kuwatengenezea wenzake nafasi za kufunga kama playmaker lakini uwezo mdogo wa kufunga ndicho kitu kinamfanya waalimu wengi kushindwa kumvumilia mchezaji huyo aliyezaliwa mwaka 1992 nchini Liberia. 

Kpah aliitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Liberia al maarufu kama ' lone star ' mwaka 2014 na mara ya mwisho ni mwaka jana mwezi juni akiwa na na kikosi cha Mpumalanga nchini Afrika Kusini.

Dumlupnar wana imani na mshambuliaji huyo kuwasaidia katika ligi yao wakikumbuka makali yake mwaka 2012-13 akibeba kombe na klabu ya nchini humo inayoitwa Centikaya TSK na kuibuka mfungaji bora na ndipo Yanga SC walipomuona na kumsajili msimu wa 2014-15 baada ya kupoteza kombe mbele ya Azam FC msimu wa 2013-14.

Licha ya kuonesha kiwango duni lakini Kpah Sherman alibahatika kuwepo katika kikosi cha mabingwa wa ligi kuu nchini msimu huo Yanga SC 2014-15 chini ya Hans Van Pluijm.

Huyo ndio Kpah Sherman na harakati zake uwanjani kijana aliyezaliwa katika mji mkuu wa Liberia , Monrovia lakini sehemu kubwa ya maisha yake ya soka akiyatumia nchini Cyprus.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top