Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: KOCHA JOSE MOURINHO AFICHUA SIRI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa Man United Jose Mourinho ameelezea kwa nini alivaa "Tracksuit" katika mechi dhidi ya Chelsea mwezi uliopita ambapo Man U...


Kocha wa Man United Jose Mourinho ameelezea kwa nini alivaa "Tracksuit" katika mechi dhidi ya Chelsea mwezi uliopita ambapo Man United walishinda 2-0, mechi hiyo ilichezwa Old Trafford.

Mourinho amekuwa kocha wa Chelsea kwa vipindi viwili ,ambapo amefanikiwa kuchukua vikombe vitatu vya EPL, FA Cup na Kombe la ligi mara 3.

Mou ameiambia BT Sport : " Nilikuja na Tracksuit , ambapo mara nyingi sifanyi hivyo. Nilifanya vile kwa sababu ilikuwa ni dhidi ya Chelsea na nilitaka kuweka wazi mimi si Chelsea hata kidogo. Chelsea ipo katika historia yangu , nipo katika historia ya Chelsea, nina heshima kubwa kwa mashabiki,walinipa mambo mengi, lakini  Mimi si Chelsea tena.
.
"kwa hiyo nilikuja na Tracksuit kwa sababu ilikuwa na Beji (Ya Man United) na kuweza kuonesha kwa kila mtu hisia zangu.
Nilifanya kwa sababu nilitaka kumaliza muunganiko wangu na Chelsea.

Kama siku moja sitokuwa Man United, na kwenda katika klabu nyingine Nitafanya hivyo hivyo. Kwa sababu tu ya kuwa Super Professional."
.
Mou Katika Msimu wake wa kwanza ameiwezesha Man United kuchukua ngao ya hisani, Kombe la ligi na Kombe la Europa League na kuiwezesha timu hiyo kufuzu michuano ya Klabu bingwa Ulaya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top