Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SIRI YA USHINDI WA REAL MADRID JANA YAFICHUKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
na Samuel Duru za uchunguzi zinaonesha ushindi wa Real Madrid jana dhidi ya Juventus jana umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Andrea Agnell r...

na Samuel

Duru za uchunguzi zinaonesha ushindi wa Real Madrid jana dhidi ya Juventus jana umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Andrea Agnell raisi wa Juventus ambaye pia ni boss wa kampuni ya FIAT.

Nyepesi nyepesi zinatanabaisha kwamba ushindi wa Real Madrid ni matokeo ya ahadi yake aliyoitoa dhidi ya wachezaji wa Juventus kwamba endapo jana wangefanikiwa kuchukua ubingwa , angempa kila mchezaji gari jipya aina ya Ferrari. Baadhi ya wadau wa soka Ulaya na sehemu mbalimbali duniani wanahisi boss huyo alitoa ahadi hiyo kimzaha na hakuamini kama timu yake ingeweza kuibuka mabingwa katika fainali hiyo.

Kipindi cha pili Juventus waliingia uwanjani wakiwa hoi bin taabani na kushindwa kabisa kuonesha upinzani kwa wakali hao wa Uhispania na kujikuta wakichapwa bao 3 baada ya sare ya 1-1 mpaka kipindi cha mapumziko.

Wadadisi wa mambo ya hujuma katika soka wanahisi baadhi ya wachezaji wa Juventus walicheza chini ya kiwango kipindi cha pili na wanataka uchunguzi ufanyike kama kuna uhusiano wowote na ahadi aliyotoa raisi wao.

Gari jipya la Ferrari kwa mwaka huu wa 2017 ni kati ya dola za kimarekani 188,425 mpaka 400,000.

" Ferrari is an Italian sports car manufacturer that specializes in high-performance luxury vehicles. Ferrari models are known for their sleek design, speed, and high sticker prices. Ferrari car prices range from $188,425 and go upwards of $400,000."

Utajiri wa Andrea Gnell kwa takwimu za mwaka 2014 na mwaka jana 2016 zinaonesha una thamani ya dola za kimarekani bilioni 13.5 . Utajiri huu unawafanya wadau wengine kupinga tuhuma hizo wakiamini ' kibopa ' huyo angweza kuwanunulia magari hayo wachezaji hao .

Ukichukua thamani ya juu kabisa ya manunuzi ya gari jipya la Ferrari kwa mwaka huu ambayo ni USD 400,000/- ukazidisha mara 33 idadi ya wachezaji wa Juventus msimu huu , unapata USD 13.2M kitu ambacho tajiri huyo angeweza kununua na kutimiza ahadi yake.

Uwezo waliouonesha Juventus katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Monaco ndio uliowapa kiburi mashabiki wa Juventus kuamini wangeifunga Real Madrid ambao walipitia moto mkali kwa wapinzani wao Atletico de Madrid.

Bado tajiri huyo wa Juventus na mmoja wa bodi ya wakurugenzi wa FIAT nchini Italia hajajibu tuhuma hizo ingawa benchi la ufundi la Juventus limesema ni upuuzi uliopindukia kuamini taarifa hizo .

Jana mapema mlinzi wa Juventus Dan Alves alitoboa siri ya ahadi ya raisi wao kuwapa bonus ya Ferrari jipya kila mmoja endapo wangeshinda mechi ya jana dhidi ya Real Madrid.

"Juventus defender Dani Alves has revealed that President Andrea Agnelli will give every player in the squad a Ferrari if they defeat Real Madrid to win the Champions" mtandao wa the Turff unatanabaisha stori hiyo.

“The only extra motivation you can do is that the president said there might be some red riding horses coming around,”Alves told the press.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top