Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: UNAMJUA MCHEZAJI WA KWANZA KUPIGA HAT TRICK KWENYE KOMBE LA DUNIANI?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa kwanza  kufunga magoli matatu katika mechi moja ya soka ( hat trick ) ni gwiji Bert Patenaube toka Marekani ( USA ). Bert alif...


Mchezaji wa kwanza  kufunga magoli matatu katika mechi moja ya soka ( hat trick ) ni gwiji Bert Patenaube toka Marekani ( USA ).

Bert alifunga magoli hayo katika fainali za kwanza kabisa za kombe la dunia zilizofanyikia nchini Uruguay. Bert alifunga magoli hayo dhidi ya Paraguay hii ilikuwa mwaka 1930.

Magoli hayo aliyafunga katika dimba kongwe la Estadio Gran Parque Central lililopo katika jiji la Montevideo mji mkuu wa Uruguay. Rekodi hiyo iliwekwa tarehe 17 julai 1930. Matokeo ya mwisho yakiwa 3-0.

Katika historia ya mchezaji huyu ambaye yupo katika orodha ya magwiji wa soka waliowahi kutokea katika taifa la Marekani ijulikanayo kama United States Soccer Hall of fame , ana historia ya kuvutia katika kuzaliwa kwake na kufa kwake.

Alizaliwa Novemba 4 1909 na kufariki pia Novemba 4 1974. Na wakati akicheza soka alikuwa akitumia namba 4 mgongoni.

Katika fainali hizo za mwaka 1930 aliongoza kwa ufungaji katika kikosi cha USA na pia kuibuka mfungaji bora wa michuano baada ya kutupia nyavuni goli 4. Goli la kwanza alifunga dhidi ya Ubelgiji 1-0 , akapiga hat trick katika mchezo dhidi ya Paraguay 3-0 kabla ya kukutana na kichapo cha 2-0 dhidi ya Argentina kwenye nusu fainali.

Baada ya michuano hiyo wamarekani hao walikwenda Brazil kwa mwaliko maalumu kucheza na wakali hao wa Latin ' selecao ' katika mchezo ambao walipigwa 4-3. Katika mchezo huo Bert alifunga magoli mawili na kuhitimisha safari yake ya kuichezea Marekani baada ya kukosa nafasi ya kuitwa tena katika kikosi hicho pia mwamko mdogo wa soka nchini humo. Hivyo katika historia yake na kikosi cha Marekani alipiga goli 6 tu katika mechi 3 alizoichezea timu hiyo.

Imeandaliwa na ;
Samuel Samuel

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top