LIGI KUU ENGLAND: EVERTON YAITWANGA QPR!
BAO safi la Shuti la Mita 20 la Ross Barkley limewabeba Everton na kuwapa ushindi wa Nyumbani Uwanjani Goodison Park walipoichapa QPR Bao 3-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa pekee Jana Usiku.
Everton walikwenda Haftaimu waiwa Bao 2-0 baada ya Frikiki ya Kevin Mirallas kuwapa Bao la Pili na Kipindi cha Pili Steven Naismith alipiga Bao la 3 kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Aiden McGeady.
Bao pekee la QPR lilifungwa na Bobby Zamora alietoka Benchi.
MAGOLI:
Everton 3
-Barkley Dakika ya 33
-Mirallas 43
-Naismith 53
QPR 1
-Zamora Dakika ya 80
Ushindi huu umeiweka Everton Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 21 zikiwa ni Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea wakati QPR wapo Nafasi ya 18, ikiwa ni Nafasi ya 3 toka mkiani, wakiwa na Pointi 14 tu.
VIKOSI:
Everton: Howard; Coleman, Jagielka, Distin, Baines; Besic, Barkley; McGeady (Pienaar - 73'), Naismith, Mirallas (Koné - 91'); Lukaku (Eto'o - 77')
Akiba: Robles, Eto’o, Kone, Pienaar, Stones, Garbutt, Alcaraz.
QPR: Green; Isla, Onuoha, Dunne, Yun; Phillips (Zamora - 59'), Mutch, Barton, Fer (Kranjcar - 77'), Hoilett; Vargas
Akiba: Ferdinand, Hill, Wright-Phillips , McCarthy, Kranjcar, Henry, Zamora.
Referee: Neil Swarbrick
Post a Comment