Katika mechi hii ambayo ilikuwa na vioja kuanzia nje ya uwanja ambapo kama kawaida makocha hao hawakupeana mikono kama ilivyo kawaida yawo ambapo mechi hii iliweza toa kadi nyekundu mbili ambazo zilikuwa za upande mmoja na maanisha Arsenal.
Kadi ya kwanza ilimkuta beki wa asernal kijana mdogo kutokea brazil Gabriel Paulista iliotokana na kumfanyia faulo striker wa chelsea Diego Costa kwa kumpiga teke kwa nyuma baada ya kuwa ameshapewa kadi ya njano sekunde chache.
Kadi nyingine alipewa kiungo wa asernal tena kipindi cha pili baada yakumchezea rafu mbaya mchezaji wa chelsea ambayo ilimfanya apewe kadi ya pili ya njano na kuwafanya asernal wabakie nane uwanjani na kuipa chelsea nafasi yakuongeza goli la pili kupitia kiungo mkabaji Matic baada goli la kwanza la chelsea kufungwa na beki Zuma.
Kwa kweli kwa kufungwa kwa Asernal leo hii mimi naona lawama kubwa sana apewe mzee Wenger maana alikuwa na mda mwingi na pesa nyingi za kusajili watu wenye akili na ambao wanaweza kumpa ushindi muda wowote ule na kwenye mechi yeyote ile.
Diego costa atapewa sifa kwa sababu aliwezatumia vyema uproffesional wake kwa kumgasi beki wa asernal ambae naye kwa utoto wake na kumfanya afanye kitendo cha kumpiga teke diego costa ambalo lilimpelekea kupata kadi nyekundu na ivyo asernal na Wenger wao kutoka kichwa chini na kuwafanya chelsea kuibuka na point zote tatu za mchezo huo.
Post a Comment