Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TUMECHOKA UWONGO WENU WENU KEANE VS HAALAND
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
September 1997 wakati Alf-Inge Haland yupo Leeds United, wanakutana na Manchester United na Haaland anamchezea Roy Keane rafu mbaya ...


September 1997 wakati Alf-Inge Haland yupo Leeds United, wanakutana na Manchester United na Haaland anamchezea Roy Keane rafu mbaya inayomfanya Keane augulie maumivu kwa muda mrefu pale chini Wakati Roy Keane anaugulia maumivu, Haland anamfuata na kumuambia ainuke kwa vile anajifanyisha kama kaumia sana, mwisho wa siku Keane anatolewa uwanjani kwa kubebwa kwenye machela, Haland analambwa kadi ya njano na dakika 90 Man U anapigwa 1-0 na Leeds United Rafu hiyo inamuweka Roy Keane akijiuguza karibu mwaka mzima huku Haland akiendelea na maisha yake ya soka kwa furaha bila wazo lolote kuhusiana na maisha ya Keane baada ya kumuumiza Maisha yanaendelea na Haland anahamia Man City,huku Keane akiwa amepona wanakutana tena uwanjani kwenye mechi ya derby kati ya Man Utd na Man City Hii mechi ilichezwa April 2001 ikiwa ni miaka mitatu na nusu ikiwa imepita tangu Haland amchezee Keane ile rafu iliyomsumbua akiwa anajiuguza karibu mwaka mzima Katika mechi hiyo iliyoishia 1-1 pale Old TraffordRoy Keane anamchezea Haland rafu mbaya inayomfanya refa ampe Keane red card, baada ya Keane kupewa red card anamfuata Haland pale chini na kuanza kumfokea kuwa ajikaze na siyo kulia kama siyo mchezaji mpira.


Baada ya mechi FA wanamuona Keane akiwa na hatia, anafungiwa mechi 3 na kumtoza paundi 5000 kama adhabu 2000 Roy Keane anaachia kitabu ambacho ndani yake alitoa maelezo kuwa rafu aliyomchezea Haland ilikuwa ya makusudi na wala hajutii kumchezea hiyo rafu mbaya kwa vile ni kitu alichokuwa amedhamiria kwa miaka mingi mno! FA baada ya kuona maelezo hayo inaamua kumpa tena adhabu ya kumfungia Roy Keane mechi 5 na faini ya paundi 150,000 Baada ya hiyo rafu Haland anaanza kuwa katika kipindi kigumu kutokana na kuumwa mguu mara kwa mara, kiasi kwamba anatumia muda mwingi akiuguza majeraha yake...July 2003 Haaland anatangaza rasmi kustaafu soka 2007 Haland anawaita waandishi wa habari na kuwaambia kuwa alishindwa kuendelea kucheza mpira kutokana na rafu ya Roy Keane, alisema hivyo kwa kuwa mwanzoni alisema kuwa Keane aliuchezea rafu mguu wa kulia ambao haukuwa na tatizo ila tatizo lilikuwa mguu wa kushoto ambao ulikuwa unamsumbua kwa muda mrefu Japokuwa alikuwa anapinga hilo suala, madaktari walimuambia chanzo cha tatizo lilikuwa rafu ya Keane...baada ya kubisha ilibidi 2007 akiri kuwa ni kweli rafu hiyo ya Keane ndiyo ilikuwa chanzo cha yeye kuharibikiwa kwenye maisha yake ya soka Thanks Roy Keane.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top