Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: CHELSEA WA MTETEA MOURINHO LICHA YA MASAIBU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chelsea imesema inamuunga mkono meneja Jose Mourinho baada ya klabu hiyo kukumbana na mwanzo mbaya zaidi wa ligi tangu 1978-79. Klabu ...

Chelsea imesema inamuunga mkono meneja Jose Mourinho baada ya klabu hiyo kukumbana na mwanzo mbaya zaidi wa ligi tangu 1978-79.
Klabu hiyo ilijipata nambari 16 ligini ikiwa na alama nane baada ya kulazwa 3-1 na Southampton Jumamosi.
Baada ya kichapo hicho, Mourinho aliambia Sky Sports kuwa klabu hiyo italazimika kumfuta kazi iwapo inataka aondoke.
"Klabu hii ingependa kuweka wazi kwamba Jose anaendelea kuungwa mkono kikamilifu,” klabu hiyo ilisema kupitia taarifa fupi.
"Tunaamini tuna meneja afaaye na awezaye kubadili hali na kwamba ana wachezaji wa kufanya hilo.”
Baada ya mabingwa hao wa Ligi ya Premia kushindwa Jumamosi, Mourinho alisema: "Ninataka kusema wazi. Mwanzo, kwamba mimi si mtu wa kukimbia.
“Pili, iwapo klabu inataka kunifuta lazima inifute lakini mimi sitoroki majukumu yangu au timu yangu.”
Chelsea walichapwa 3-1 na Southampton Jumamos
Hayo yakijiri, nahodha wa klabu hiyo John Terry pia amesema Mreno huyo wa umri wa miaka 52 ndiye afaaye Zaidi kusaidia klabu hiyo kujikwamua.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top