El Derbi Madrileno, Mechi ya Mahasimu wa Jiji la Madrid
huko Spain, Atletico Madrid na Real Madrid, iliyochezwa Vicente Calderon
imemalizika kwa Sare ya 1-1.
Real walitangulia kufunga katika Dakika ya 9 baada ya Krosi
ya Carvajal kuunganishwa kwa Kichwa na Karim Benzema na kumwacha Kipa
wa Atletico Oblak akidaka hewa.
Katika Dakika ya 20 Atletico walipewa Penati kufuatia rafu
ya Ramos kwa Tiago na Griezmann kupiga Penati hiyo ambayo Kipa wa Real
Navas aliikoa.
Hadi Haftaimu, Atletico 0 Real 1.
Bao la kusawazisha la Atletico lilifungwa Dakika ya 84 na
Luciano Vietto, Mchezaji alietokea Benchi Dakika ya 58 kumbadili Angel
Correa.
Matokeo haya yamewapaisha Real na kukamata Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Villareal.
VIKOSI:
Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Gimenez, Godin, Filipe; Tiago, Gabi, Oliver; Griezmann, Torres, Correa.
Real Madrid: Navas; Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modric; Isco, Ronaldo, Benzema.
LA LIGA MATOKEO:
Ijumaa Oktoba 2
Celta de Vigo 0 Getafe CF 0
Jumamosi Oktoba 3
Sevilla FC 2 FC Barcelona 1
Granada CF 1 Deportivo La Coruna 1
RCD Espanyol 1 Sporting Gijon 2
Las Palmas 0 SD Eibar 2
Malaga CF 3 Real Sociedad 1
Jumapili Oktoba 4
Rayo Vallecano 0 Real Betis 2
Athletic de Bilbao 3 Valencia C.F 1
Levante 1 Villarreal CF 0
Atletico de Madrid 1 Real Madrid CF 1



Post a Comment