Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano
na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume,
ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa
Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akiongea na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza
kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia
moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668
(Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji,
uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa
ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika
mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze
kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa
Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya
vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman
kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira
miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia
kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14
Novemba, 2015
KAMATI STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI
Title: KAMATI STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karum...



Post a Comment