Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: STARS VS THE FLAMES
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
The flames wanaotamba na mfumo wa 4_1_2_3  wakimtegemea Joseph Kamwendo toka TP Mazembe nafasi ya kiungo ya chini , watakwaana na miamb...
The flames wanaotamba na mfumo wa 4_1_2_3  wakimtegemea Joseph Kamwendo toka TP Mazembe nafasi ya kiungo ya chini , watakwaana na miamba ya taifa Stars chini ya Boniface Mkwasa ambaye anaonekana kujiamini sana na kikosi chake .
Taifa Stars almaarufu kama JK boys au ukipenda waite " the blues of Africa " hawana cha kupoteza leo mbele ya wanyasa hao.


Boniface the master of wide formations in Tanzania leo anaweza akaja na 4_3_3 , 4_2 _3_1  ama akawaacha Ngasa na  Samata waunganishe nguvu mbele chini wakipewa back up na Ulimwengu katika 4_2_1_3.


   Chachu ya mkataba mnono jana inampa hamasa Mkwasa kukipanga kikosi vyema lakini pia kuimarika kwa Ngasa, Mwinyi Kazimoto na ukali wa Samata katika utupiaji vinazidi kuipa turufu stars.


  Wanaume 11 uwanjani watachagizwa na hamasa za mamia ya watanzania wakiongozwa na group maarufu la Taifa Stars Supporters lililojiandaa vyema kuwapa ari , motisha na hamasa vijana wetu.
Tahadhari kubwa kwa stars ni uchezaji wa the flames hasa wanapomaliza half line, huingia kwa kasi kwa pasi fupi fupi ama long balls kupitia flanks wakiwategemea washambuliaji wao maarufu kama Robinson Ngalande,  Nyondo na Chiukepo wakipikiwa vyema na Midfielders zao kama Joseph Banda , Frank Banda na yule mwenye kasi ya ajabu mtaalamu wa switching Chimango Kayira dogo wa mwaka 1993 .

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Taifa Stars

Samuel Samuel

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top