Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TEGETE AWA MCHEZAJI BORA WA WIKI WA LIGIKUU YA VODACOM TANZANIA KUPITIA TOVUTI YA GOAL.CO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
mchezaji bora wa wiki wa Ligi kuu Tanzania bara Tegete amefikisha mabao matatu katika mechi mbili alizoichezea timu hiyo Mshambuliaji w...
mchezaji bora wa wiki wa Ligi kuu Tanzania bara

Tegete amefikisha mabao matatu katika mechi mbili alizoichezea timu hiyo
Mshambuliaji wa Mwadui FC, Jeryson Tegete ndiyo mchezaji bora kwa mechi za Ligi ya Vodacom kwa wiki hii baada ya kuifungia timu yake mabao 2 katika ushindi wa mabao 3-1, iliyoupata Mwadui ilipocheza na Mgambo JKT jana mkoani Shinyanga.
Tegete aliyeichezea Yanga kwa mafanikio makubwa kabla ya kocha Hans van der Pluijm, kuamua kumtema kwenye kikosi chake cha msimu huu kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza ameonekana kurudi kwenye kiwango chake kilichozoeleka baada ya Jumamosi iliyopita kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1, walioupata dhidi ya JKT Ruvu.
Kocha wake wa sasa Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema kasi ya Tegete imempa matumaini ya kupata ushindi zaidi katika mechi zijazo na anaimani kubwa na mshambuliaji huyo kuwa anauwezo wa kurudi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania inayofundishwa na kocha mzawa Boniface Mkwassa.
Kwa sasa Tegete amefikisha mabao matatu katika mechi mbili alizoichezea timu hiyo ikiwa ndiyo kwanza anaingia kwenye kikosi cha kocha Julio, baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiunguza majeruhi ya nyama za paja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top