Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: LEICESTER CITY YAKWAA KISIKI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Liverpool wamepunguza kasi ya Leicester kileleni mwa Ligi ya Uingereza baada ya kuwalaza 1-0 uwanjani Anfield. Leicester walikuwa wameenda ...

Liverpool wamepunguza kasi ya Leicester kileleni mwa Ligi ya Uingereza baada ya kuwalaza 1-0 uwanjani Anfield.
Leicester walikuwa wameenda mechi tisa bila kushindwa ligini na leo imekuwa mara yao ya kwanza kumaliza bila kufunga bao ligini msimu huu.
Uwanjani Britannia, masaibu ya meneja Louis Van Gaal yamezidi baada ya Red Devils kucharazwa 2-0 na Stoke City. Meneja huyo amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
Tottenham Hotspur nao wamefufua juhudi zao za kupigania taji la ligi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Norwich City, wakisaidiwa sana na kipa Hugo Lloris anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.
Na uwanjani Stamford Bridge, hakukuwa na habari njema sana kwa kaimu meneja Guus Hiddink baada ya vijana wake wa Chelsea kutoka sare ya 2-2 na Watford.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, aliyewafungia mabao yote mawili pia ameonyesha kadi ya manjano, hii ikiwa na maana kwamba hataweza kuwachezea dhidi ya Manchester United Jumatatu 28 Desemba.
Kiungo wao wa kati Oscar alipoteza nafasi nzuri ya kuwaweka kifua mbele alipoonekana kuteleza na kupoteza mkwaju wa penalti dakika za mwisho za mechi.
Kwa Manchester City uwanjani Etihad, ilikuwa siku ya mavuno, klabu hiyo ikipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Sunderland licha ya Wilfried Bony kupoteza mkwaju wa penalti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top