4. ANTHONY MARTIAL wa Man United licha ya kuwa na umri wa
miaka 19, uwezo na umahiri wake wa kucheka na nyavu
unaaminika kuwa utakuwa na kumfanya awe mchezaji bora
wa dunia, kwani uwezo wake anaouonesha sahizi unafanya
wengi kutarajiwa makubwa kutoka kwake.
3- EDEN HAZARD wa Chelsea ambaye alishinda tuzo ya
mchezaji bora wa msimu kwa msimu uliyopita, alionekana
kuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi kuliko
kufunga, hilo linatajwa kuwa suala la mpito ila uwezo wake
mkubwa unfanya watu wamtabirie makubwa.
2- LUIS SUAREZ
Baada ya majina matatu ya mwisho ya wanaowania tuzo ya
mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2015 kutajwa, wakiwa
Neymar , Messi na Ronaldo , staa wa soka wa Brazil Neymar
ndio alikuwa wa kwanza kutoka hadharani na kusema kuwa
Luis Suarez alistahili kuwepo miongoni mwa majina matatu.
1- NEYMAR JR
Ni ukweli usiofichika kuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo
wanabidi wajipange kwa staa wa soka wa Brazil na nahodha
wa timu hiyo Neymar , kwani anaonekana kuja juu kwa kasi.
Neymar katika umri wake wa miaka 23, amefanikiwa kufunga
magoli 209 katika michezo 341 kwa vilabu vyote alivyowahi
kuchezea. Hii ni dalili ya nyota huyo kuja kufanya vizur kwa
siku za karibuni.


Post a Comment