Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre Can ukipanguliwa na kipa David De Gea.
Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.
Wageni hao ambao sasa wako katika nafasi ya tano walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.
Liverpool itasalia katika nafasi ya tisa ikiwa alama sita nyuma ya Manchester United.
Mambo matano usiyoyajua tokana na mchezo huo.
● Manchester United Imefunga bao la 100 katika uwanja wa Anfield tangu timu hizo zilipoanza kukutana.
● Wayne Rooney amefikisha magoli 176 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi akiwa na klabu moja katika EPL
● Liverpool ndiyo klabu iliyofungwa magoli mengi kwa mipira ya kona katika EPL ikiwa imefungwa magoli 7 msimu huu.
● Man United imefunga katika mashuti manne waliyopia golini katika mechi zote mbili dhidi ya Liverpool msimu huu.
● Kocha Van Gaal ameshinda mechi zote nne alizocheza dhidi ya Liverpool
Post a Comment