Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MATUMAINI YA CANAVARO KUREJEA BADO NI NDOTO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Matumaini ya kurejea mapema uwanjani kwa nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yamefutika kufuatia majibu ya vipimo kuonyesha kuwa bad...

Matumaini ya kurejea mapema uwanjani kwa nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yamefutika kufuatia majibu ya vipimo kuonyesha kuwa bado hajapona majeraha yake.

Cannavaro yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya kisigino.

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, alisema wamemfanyia vipimo kwa mara ya pili beki huyo lakini inaonyesha bado hajapona vizuri huku wakiwa hawajui lini ataweza kurejea uwanjani mpaka atakapoonana na daktari bingwa wa mifupa.

“Baada ya kumfanyia tena vipimo, tumegundua bado hajapona vizuri, kwa hiyo tumemuwekea bandeji ngumu (P.O.P) nyingine, lakini pia tumempa programu ya kuonana tena na daktari bingwa wa mifupa kwa sababu alichoumia ni mfupa wa kisigino.

“Unajua ameumia muda mrefu tangu Mei 15, mwaka jana, tumekuja kugundua tatizo baadaye sana, tukamuwekea P.O.P ila mifupa haijaunga vizuri, kuhusu lini atarejea, subiri mpaka tupate majibu ya daktari bingwa mara baada ya kumcheki,” alisema Matuzya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top