1. Deogratius Munishi " Dida"
Wakati alipowekwa benchi baada ya kuanza kufungwa magoli ya aina moja hususani mashuti ya mbali na free header, nadhani alijiuliza sana na kuanza kufanyia mazoezi . Hongera Sana Juma Pondamali. Amesimama vyema langoni na kuipanga beki yake vyema. Kipindi cha kwanza Majimaji walipata clear chances 3 na zote alizicheza. Mechi hii inampa 8 Clean sheets toka arudi golini.
2. Juma Abdul / Salumu Telela
Huyu ni injini ya kulia ya Yanga , aliweza kuwadhibiti majimaji upande wa kulia kabla ya kuumia. Bado ni msaada mkubwa katika kusaidia mashambulizi wing ya kulia . Kocha alipomtoa nje na kumleta Telela kushika nafasi hii ya kulia kiasi kupanda na kushuka kulipungua lakini Abo Master still aliweza kujenga kombinesheni nzuri na walinzi wa kati.
3. Oscar Fanuel Joshua
Nadhani leo Pluijm amefurahi sana kwa soka zuri lililooneshwa na mlinzi huyu wa kushoto. Ni nadra sana kumuona Oscar anapanda na kushuka na kutoa assist kwa washambuliaji wa kati lakini leo Oscar amewamudu vyema Majimaji, ametoa pasi ndefu, kasi na kipindi fulani kutoa back up nzuri kwa walinzi wa kati.
4. Kelvin Yondani.
Amecheza kama sweeper , ameonesha bado ni moyo wa safu ya ulinzi wa kati. Kizuri kwake nikuwa aware muda wote. Hata wakati washambuliaji wa kati walipofanikiwa kumzidi Bossou alifika na kutoa back up. Technical Clearance na hata alipoingia Makapu kama defensive midfielder alikuwa anapanda kuhakikisha Dida yupo mbali na hatari zote za Majimaji.
5. Vicente Bossou
Ni moja kati ya mechi ambazo zimeonesha uzuri wake hasa katika utulivu wa kupambana na washambuliaji wa kati. Ni mtulivu sana hasa anapofanya clearance . Ni nadra sana kumuona anabutua mbele hata kama yupo under pressure . Anapenda kutoa padi kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi toka nyuma . Anakosa kitu kimoja tu ambacho ni common kwa walinzi wa kati. He is not aggressive.
6. Salumu Telela / Juma Makapu
Telela ni mmoja wa viungo wakabaji wazuri sana hasa katika blocking , cut off na kusambaza mipira tokea kati huku akimpa kiungo wa mbele uhuru mzuri wa kuichezesha forward line. Dakika 15 za mwanzo walisimama vyema na kamusoko na kuwafanya Majimaji kukimbia kati na kuhamia upande wa kulia lakini bado Telela amepunguza kasi nadhani benchi na majeraha yamechangia. Walipofanya rotation na Makapu ndipo kwa asilimia 100% kiungo cha chini cha Yanga kilipotulia. Makapu ni mzuri sana katika kukaba, kutibua na kuanzisha mashambulizi ya kasi kutokea kati nasubiri siku atakayo master kupiga straight deep passes kwa forward ili kutimia kama kiungo mkabaji tegemeo . Ujio wa Makapu pale kati ulitengeneza kombinesheni nzuri sana kati ya Kamusoko aliyecheza kama free midfielder, Ngoma ambaye leo ni man of the match kwa kusimama kama play maker na Tambwe . Kama ulikuwa makini kasi ya forward line ya Yanga ilitokana na base nzuri ya mashambulizi tokea kati hali iliyowafanya Majimaji kurudi nyuma na muda wote kuwa under pressure tactically.
7. Saimoni Msuva
Wengi wanatamani wamuone akitoka na goli uwanjani. Anakosa umakini lakini sasa naanza kumuelewa licha ya kupoteza nafasi nyingi lakini Msuva ndio chachu ya kukumbusha backline ya timu pinzani kwa sasa. Muda wote yupo aggressive and speedy. Hali hii inawalazimisha mabeki muda wote kumchunga. Utakuta anapewa marking na watu si chini ya wawili hali ambayo inaondoa tactical ratio katika marking zone hivyo baadhi ya wachezaji kuwa free out of screening or marking. Hii imempa advantage sana Tambwe ambaye ni mzuri kujificha na kuibuka kwenye move . Tazama goli la tano alivyoibuka very unexpectedly na kutia goli.
8. Thabani Kamusoko
Leo mwalimu katumia 4-3-3 kama kawaida na muhimili wa mfumo huu ulikuwa unalindwa vyema na mtaalamu huyu. Niliwahi kusema si mzuri kwenye marking kwa maana nzima ya kusimama kama defensive or destroyer midfielder lakini ni mzuri kusimama kiungo wa mbele. Leo akiwa na Makapu na hata mwanzo Telela ameonesha uwezo mzuri sana wa kuituliza timu kufanya mashambulizi ya maana. Kila akipata mpira husogea kwenye attacking zone akiwa kasi lengo ni kuwarudisha nyuma walinzi wa kati wa timu pinzani defensively imbalance ili atakapotoa pasi ya mwisho wasiweze ku intercept au kumfanyia screening attacker. Kamusoko anajua kumchezesha Ngoma ama Tambwe kwa kuruhusu uwiano mzuri wa kiungo na safu ya ushambuliaji. Lakini tazama alivyofunga goli la kwanza. Ni akili ya mpira iliyomfanya atulie na kutengeneza bending shot ili mpira usipae ( accuracy) . Ball brain . He can change as attacking midfielder accordingly.
9. Amisi Tambwe.
Master of hat trick. Mwanzoni kabisa Majimaji hawa kumpa concentration walijikita sana kumfanyia cutt off kwa walishaji wake. Wakimbana Kaseke, Msuva , wings zote na kuhakikisha hakuna playing combination ya yeye na Ngoma . Hili Kamusoko aliliona akaanza kuongeza pressure yeye na Kaseke ili walinzi wa Majimaji warudi kwenye muhimili wao na kuacha man to man defense na kurudi kwenye zonal marking na kidogo man to man kwa key players . Hapo ndipo Tambwe alipoanza kukaa njiani in a stealth way na kufanikiwa kupiga hat trick kama center forward. Mzuri sana kwa mipira ya vichwa ya aina yote.
10. Donald Ngoma
Naweza sema huyu ndio man of the match . Licha ya kufunga goli la pili huku akicheza kama second striker , Ngoma pia amesima kama play maker katika forwad line . Amempa assist za kutosha Ngoma . Tazama goli la nne alikuwa kwenye impossible angle lakini baada ya kuutuliza mpira hakuwa mchoyo na kumtengenezea pasi nzuri Tambwe ya goli. Kila siku anaonesha umuhimu wa timu work huku fighting spirit yake ikiwa juu sana . He is always keeping the backline busy . Hii ni faida kubwa sana katika timu yakuwa na mtu kama huyu.
11. Deusi Kaseke
Kuaminiwa kikosi cha kwanza kunamjengea kujiamini katika kikosi cha mdachi huyo. Ana uwezo mzuri wa kupokonya mipira na kutoa pasi nzuri. Leo alikuwa katika ubora wake ule uliomfanya wana Mbeya City kumuita Iniesta . Aliweza kujaribu kutengeneza krosi nzuri za juu na hata walipofanya swamping na Msuva na yeye kuja kulia bado alionesha uimara bado hajawa bora sana kutoa pasi na krosi kwa wakati licha ya wakati fulani kusimama kama kiungo mshambuliaji wa pembeni na kufanya attempt mbili za maana.
Kutokea Sub:
1. Issoufou Boubacar
Bado kile wanajangwani wanachokitaka hawajakiona kwa uzuri. Ni mchezaji mzuri kwenye holding , kupiga krosi na kupiga fouls lakini anakosa kasi .
Team work:
Yanga walkuwa vizuri kisaikolojia na hasa baada ya kupata goli la kwanza lakini kujiimarisha kwa Majimaji kulianza kuwatoa mchezoni na kujikuta wanashambulia bila malengo hususani wing ya kulia .
Kipndi cha kwanza walikuwa wanaanzia kushambulia kutoa nyuma na wakifika mbele tayari Majimaji wanawatoa kwenye mchezo.
Kipindi cha pili Yanga walirudu na mbinu ya kufanya mashambulizi ya kasi kuanzia katikati na wakienda aggressively from all angles. Mashambulizi hayo toka pande zote yaliwafanya Majimaji kurudi nyuma na kuwaruhusu Yanga kuwashambulia muda wote na ndipo walipopata magoli yote manne.
Asanteni:


Post a Comment