Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: KARIBU EPL PEP GURDIOLA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pep ni mmoja wa makocha bora wa dunia kwa sasa. Lakini changamoto ambayo atakabiliana nayo kutoka England inaweza kuwa kubwa kwake sababu a...

Pep ni mmoja wa makocha bora wa dunia kwa sasa. Lakini changamoto ambayo atakabiliana nayo kutoka England inaweza kuwa kubwa kwake sababu alikotoka mara nyingi upinzani mkubwa kwake hua na mzunguko mchache(mdogo) kwa msimu nikimaanisha kipindi yupo Barcelona ni mechi mbili tu ambazo labda zilikuwa zinamnyima usingizi ni dhidi ya Real Madrid(Home and Away). Ni vivyo hivyo alivyoenda Bundesliga,alikuta wapiñzani wake hawana ubavu wa kupambana nae na ndio ilipelekea kuona Bayern Munich wanapoteza mechi 1 au 2 tu katika msimu wote.

Maisha ya ligi kuu ya Uingereza ni tofauti na yanaweza kumshangaza Pep sababu ushindani wa mataji ya ndani ni mkubwa zaidi ya alikotoka huku kuna Man Utd,Arsenal,Liverpool, Chelsea na Tottenham na wengine ambao hupenda kuharibu sherehe za watu.

Pia pale england pana vilabu ambavyo kila msimu huwa ni visiki kwa wakubwa wa ligi kuu hapa na maanisha
West ham  Hawa bwana ni vigumu sana kigogo awaye yeyote kuchukua point zote 6 toka kwao.

Sunderland Hawa pia ni wagumu sana na mara nyingi nao wamekuwa wagumu kupoteza point 6 tena pale wanapocheza na vigogo.

Epl ni mara chache sana kumaliza ujafungwa au kumaliza msimu kwa kuzifunga timu zote kama ilivyokuwa spain au German.
Epl ni ligi yenye ushindani mkubwa sana kila timu kwenye ligi ina uwezo wakuchukua point kwa mwenzake.
Naelewa kwa man city utaweza sajili aina ya wachezaji uwatakao kutokana na hela iliopo hapo lakini nakuasa tu Chelsea walikuwa na uwezo huo huo lakini bado kocha wao kipenzi Josee alitimuliwa kazi.

Pep usitegemee mteremko kabisa pale Epl angalia sana usije chafua cv yako huku mwishoni.
Karibu sana ligi kuu England ligi yenye mashabiki wengi,ligi inayotizamwa zaidi duniani na pia ligi ambayo kwa sasa inaaminika ndio ligi yenye thamani kubwa zaidi duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top