Manchester United wapo mbioni kuvunja
Rekodi ya Uingereza kwa kuwa Klabu ya
kwanza kabisa ya kuvuna Mapato ya zaidi
ya Pauni Nusu Bilioni kwa Mwaka mmoja
licha ya Timu kusuasua Uwanjani.
Sare ya 1-1 ya Jumapili iliyopita huko
Stamford Bridge na Chelsea imewaacha
wakiwa Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu
England huku wakiwa Pointi 6 nyuma ya
Timu ya 4 ambayo ndio Nafasi ya mwisho
ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu
ujao.
Pia, Man United sasa wapo kwenye uvumi
mkubwa kuwa Meneja wao, Louis van Gaal,
atabadilishwa mwishoni mwa Msimu na
Jose Mourinho.
Lakini licha ya matatizo hayo, Man United
Kibiashara imezidi kuimarika na Leo
wametangaza Mapato yao kwa Mwaka
yatagonga Pauni Milioni 500 hadi 510 kitu
ambacho hakuna Klabu yeyote ya
Uingereza imewahi kufikisha.
Mapato kwa Robo ya Pili ya Mwaka
yamepanda na kufikia Pauni Milioni 133.8
ikiwa ni ongezeko la Asilimia 26.6 kutoka
ya Mwaka uliopita wa Fedha.
Mapato kutokana na Matangazo
yamepanda kwa Asilimia 31.3 na yale ya
Udhamini kwa Robo ya Pili ya Mwaka
yamepanda kwa Pauni Milioni 1.6 na
kufikia Pauni Milioni 37.4.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Post a Comment