Yanga SC inatarajiwa kuondoka nchini Jumatano kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim uliopangwa kuanza Saa 9:30 Alasiri kwa saa za huko Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe.
Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye, Februari 27 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mara tu baada ya mchezo wa kwanza na Joachim nchini Maurtius, Yanga itarejea kwenye Ligi Kuu kwa ajili ya mchezo na mahasimu wa jadi, Simba SC Februari 20, mwaka huu Uwanja wa Taifa. Tayari michezo miwili dhidi ya Mtibwa na African Sports imehairishwa.


Post a Comment