Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SANCHEZ ASEMA UBINGWA WA EPL ASERNAL NI NDOTO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili m...

Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester United na Swansea.

The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.

''Mara nyingine tunakosa motisha kwamba tayari tumeshinda 1-0 tunapoelekea uwanjani'',aliiambia Directiv Sport kabla ya mechi dhidi ya United.''Tunakosa ile ari kwamba tunaweza kuwa mabingwa''.

Sanchez aliongea:Iwapo tutaingia katika uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.

''Ninakumbuka mechi dhidi ya Manchester United mwaka uliopita.Wachezaji walikuwa na motisha ya kushinda taji tulipoingia uwanjani.Tuliwashinda katika dakika 20 na kupata 3-0.Tulikuwa na ari na kujiamini siku hiyo''.

Arsenal imeshinda mara tatu pekee kutoka mechi 11 katika mashindano yote na wako katika nafasi ya tatu katika ligi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top