Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha
baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya
mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba
SC, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana michezo,
huku ikiwataka wanachama, washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao
waliopo madarakani na kama kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika
vilabu vyao.
Mashabiki wa klabu ya Simba walifanya vurugu kwa kurusha mawe,
wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji, magari
waliyokuwa nayo baada ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans
kwa bao 1- 0.
Jeshi la Polisi baada ya kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja
punde tu mchezo ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea
kurusha mawe hali iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya
katika eneo hilo.
Kufutia kitendo hicho, Jeshi la Polisi lilihakikisha bus la timu ya
Simba SC na viongozi wake wanaondoka salama uwanjani baada ya
kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango wa karakana ya wachina
waliojenga uwanja huo.
Aidha TFF imeviomba vyombo vya Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua
kali mashabiki waliohusika na kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni
kosa la jinai na wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
TFF YALAANI VURUGU ZA MASHABIKI
Title: TFF YALAANI VURUGU ZA MASHABIKI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchez...



Post a Comment