Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi
yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu
hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa
Jukwaa la VIP “A” kuwa ni Sh 30,000; VIP “B” na “C” Sh 20,000 wakati
jukwaa la viti Rangi ya chungwa ni Sh 7,000 wakati mzunguko wa viti vya
bluu na kijani ni Sh 5,000.
Kwa mujibu wa Muro, Yanga itawakosa wachezaji mahiri wawili, Donald
Ngoma na Thaban Kamusoko ambao watatumia mchezo huo kutumikia adhabu ya
kadi mbili za njano walizoonywa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika kabla ya kushuka kucheza Kombe la Shirikisho.
“Tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa
wingi kesho kuishangilia timu yetu kwa nguvu na kasi kubwa,” amesema
Muro ambaye alitumia nafasi hiyo kutamba kwamba Yanga ilisajili
wachezaji 24 kwenye michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani
Afrika (CAF).
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Post a Comment